Thursday, January 2, 2014

HAPPY NEW YEAR 2014!

Namshukuru Mungu kwa Mwaka 2013 kwa mema mengi alionijalia.

Mwaka 2013 ulikuwa unachangamoto nyingi sana kwangu lakini siku zote Mungu ni mwema na kila kwenye changamoto alinipa mlango wa kutokea.

Mwaka 2014 napenda kuwa Chanya kwenye kila mawazo, maneno na matendo yangu. Vitu muhimu mwaka huu navyotaka kuvifanya,

i) Nataka kujifunza kuwa karibu sana na Mungu na kuijenga Imani yangu kiroho.

ii) Nataka kuwa Mama mwema, mtoto mwema,mchumba mwema, dada mwema, shangazi mwema, rafiki mwema, jirani mwema, mfanyakazi mwema na mjasiriamali mwema.

iii) Nataka kuwa na muda mwingi na familia yangu (extended one) na watu ambao watanipenda na kuthamini upendo wangu.

iv) Nataka kuyapa uzito mambo ambayo yatajenga na kunipa furaha mimi na ninao wapenda, vingine vyote vitakavyokuwa vinanikera, kunipotezea muda , kuniweka mbali na Mungu sitataka kuvipa nafasi kabisa.

MWAKA HUU NIKO CHANYA SANA KWENYE KILA KITU KATIKA MAISHA YANGU, MUNGU  UJALIE!

Napenda kuwatakia heri ya mwaka mpya na wenye Amani, Upendo na Mafanikio Tele.

Nawapenda sana

Winnie!

Monday, October 21, 2013

HAPI BESIDEI MAI MINI MI

Na mshukuru mungu kwa siku ya tarehe kama ya leo miaka miwili iliyopita muda wa saa mbili na dakika tano asubuhi alinipa zawadi nzuri isiyo na kifani.

Ni wewe mtoto wetu Alexa Graciela. Mungu tunakushukura kwa kuwa mwema kwetu na kwa Alexa. 

Alexa tunakuombea Mungu akujalie Afya njema, Hekima, Unyenyekevu, Maarifa, Kumjua Mungu na Mengi mengi yalio mema.

Tunakupenda sana, Hapi besi dei kipenzi chetu!

Thursday, October 10, 2013

Wednesday, August 28, 2013

................ Mungu ........................................

Habari wapendwa...

Mtumikie Muumba wako siku za Ujana wako,.....................................



Nawatakia Jumatano njema!!!

Nawapenda,

Winnie!

Wednesday, August 7, 2013

Mtoto wa kiafrika..........


Habari wapendwa, 
Leo nimeguswa kuongelea mtoto wa kiafrika kwa sababu nimeshawahi kuwa mtoto wa kiafrika na kwasasa nina watoto ambao ni waafrika. Nimekuta najiuliza hivi watoto wetu ambao tunawazaa sisi wenye damu ya kiafrika kweli tunawalea kiafrika? Niweza kuwa na ujasiri wa kuongelea watoto wa kiafrika kwasababu mimi ni mwafrika, ila watoto wa kizungu ninawajua kupitia kusoma vitabu vilivyo andikwa na hao wazungu na kupitia sinema ambazo unakuta zinaelezea habari iliyowahi kutokea kweli katika maisha yao ( based on true story)
Sasa basi mtoto ni toka akiwa ndani ya tumbo la mama yake mpaka anapotimiza umri wa miaka 18 hii ni kwatafsiri ya katiba ila kwa sisi wamama ambao tunawatoto mtoto ni toka akiwa ndani ya tumbo la mama yake mpaka kiama atabaki kuwa mtoto.
 

Mama wa kiafrika tuwalee watoto wetu katika maadili na tamaduni za kiafrika ambazo ni zuri na zenye tija, hapa naanza na vyakula: tule vyakula vyetu vya kiasilia kwani nivyakula vyenye lishe na uboro wa juu ukilinganisha na vya wenzetu wazungu. ( tule matunda, mboga, nafaka, na vinywaji ambayo hayajawekewa machemiko kwa ajili ya kuhifaziwa au kutengenezwa). Na watoto wanyonye maziwa ya mama kwa muda mrefu ikiwezekana mpaka hata wakiwa na umri wa miaka miwili.

 
Malezi: malezi ya watoto wa kiafrika yanabidi kuwa yanafuata mila, desturi na tamaduni za kiafrika ambazo ni nzuri ( hapa namaanisha nizile ambazo hazitawafanya watoto kujuta kuwa wa afrika).

Nimengi yakuongea kwenye swala la mtoto wa Kiafrika, tutakuwa tunaongelea kila tutakapopata nafasi ya kuongelea. 
  Wewe unalipi la kutuambia Kuhusu mtoto wa kiafrika.......................
  
Winnie!


Thursday, July 18, 2013

Malengo/Ndoto …............


Kwenye maisha kila mtu anakuwana Malengo/Ndoto. Ni vizuri kuweka malengo/ndoto zetu kwenye maandishi ili kuwa na uwezo wa kujikumbusha kila asubuhi ambayo muuamba anakuwa ametujalia ili tujitahidi kufikia/kutimiza malengo/ndoto. Ni muhimu sana tukajiwekea na muda wa kutimiza hayo malengo/ndoto ili tuweze kuja kujipima. Tusipoweka malengo/ndoto zetu kwenye maandishi ni rahisi kuzisahau na kuzibadili na kushindwa kutimiza/kufikia.

Basi tusisahau kumtanguliza Mungu katika kila jambo.


Siku njema, nawapenda sana.


Winnie.


Monday, July 15, 2013

NIMEJIFUNZA KUKAA KIMYA NI JIBU ZURI KULIKO MAJIBU YOTE NILIYOKUTANA NAYO.
NINI MAWAZO YAKO KUHUSU HILI?