Habari wapendwa,
Leo
nimeguswa kuongelea mtoto wa kiafrika kwa sababu nimeshawahi kuwa
mtoto wa kiafrika na kwasasa nina watoto ambao ni waafrika. Nimekuta
najiuliza hivi watoto wetu ambao tunawazaa sisi wenye damu ya
kiafrika kweli tunawalea kiafrika? Niweza kuwa na ujasiri wa
kuongelea watoto wa kiafrika kwasababu mimi ni mwafrika, ila watoto
wa kizungu ninawajua kupitia kusoma vitabu vilivyo andikwa na hao
wazungu na kupitia sinema ambazo unakuta zinaelezea habari iliyowahi
kutokea kweli katika maisha yao ( based on true story)
Sasa basi mtoto ni toka
akiwa ndani ya tumbo la mama yake mpaka anapotimiza umri wa miaka 18
hii ni kwatafsiri ya katiba ila kwa sisi wamama ambao tunawatoto
mtoto ni toka akiwa ndani ya tumbo la mama yake mpaka kiama atabaki
kuwa mtoto.
Mama wa kiafrika
tuwalee watoto wetu katika maadili na tamaduni za kiafrika ambazo ni
zuri na zenye tija, hapa naanza na vyakula: tule vyakula vyetu vya
kiasilia kwani nivyakula vyenye lishe na uboro wa juu ukilinganisha
na vya wenzetu wazungu. ( tule matunda, mboga, nafaka, na vinywaji
ambayo hayajawekewa machemiko kwa ajili ya kuhifaziwa au
kutengenezwa). Na watoto wanyonye maziwa ya mama kwa muda mrefu
ikiwezekana mpaka hata wakiwa na umri wa miaka miwili.
Malezi: malezi ya
watoto wa kiafrika yanabidi kuwa yanafuata mila, desturi na tamaduni
za kiafrika ambazo ni nzuri ( hapa namaanisha nizile ambazo
hazitawafanya watoto kujuta kuwa wa afrika).
Nimengi yakuongea kwenye swala la mtoto wa Kiafrika, tutakuwa tunaongelea kila tutakapopata nafasi ya kuongelea.
Wewe unalipi la kutuambia Kuhusu mtoto wa kiafrika.......................
Winnie!
No comments:
Post a Comment