Thursday, January 2, 2014

HAPPY NEW YEAR 2014!

Namshukuru Mungu kwa Mwaka 2013 kwa mema mengi alionijalia.

Mwaka 2013 ulikuwa unachangamoto nyingi sana kwangu lakini siku zote Mungu ni mwema na kila kwenye changamoto alinipa mlango wa kutokea.

Mwaka 2014 napenda kuwa Chanya kwenye kila mawazo, maneno na matendo yangu. Vitu muhimu mwaka huu navyotaka kuvifanya,

i) Nataka kujifunza kuwa karibu sana na Mungu na kuijenga Imani yangu kiroho.

ii) Nataka kuwa Mama mwema, mtoto mwema,mchumba mwema, dada mwema, shangazi mwema, rafiki mwema, jirani mwema, mfanyakazi mwema na mjasiriamali mwema.

iii) Nataka kuwa na muda mwingi na familia yangu (extended one) na watu ambao watanipenda na kuthamini upendo wangu.

iv) Nataka kuyapa uzito mambo ambayo yatajenga na kunipa furaha mimi na ninao wapenda, vingine vyote vitakavyokuwa vinanikera, kunipotezea muda , kuniweka mbali na Mungu sitataka kuvipa nafasi kabisa.

MWAKA HUU NIKO CHANYA SANA KWENYE KILA KITU KATIKA MAISHA YANGU, MUNGU  UJALIE!

Napenda kuwatakia heri ya mwaka mpya na wenye Amani, Upendo na Mafanikio Tele.

Nawapenda sana

Winnie!

No comments:

Post a Comment